Sunday, July 20, 2014

Kahaba wa Tanzania Asimulia Jinsi alivyousambaza UKIMWI kwa Maelfu ya Wanaume; Mnaonunua hii inawahusu.


MWANAMKE mmoja wa Kitanzania aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika miji mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam na mingine ya Namibia, ameibuka na kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya kusambaza Ukimwi kwa wanaume wakware.

Licha ya kukiri kufanya hivyo, akisema kwa siku alipanga hadi wanaume watano,tena bila ya kutumia kinga akisema alidhamiria kuusambaza ugonjwa huo hatari alioambukizwa akiwa katika shughuli za ukahaba.

Binti afanyiwa mchezo mchafu chooni baada ya kulewa vibaya akiwa Night Club.



Alijigundua ameathirika mwaka 2006. Hata hivyo, katika maelezo yake ameelezea kuijutia dhamira yake hiyo, akisema alisambaza kutokana na hasira aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume aliyemwambukiza.

“Nilimchukia sana kila mwanamume, yeyote aliyejiita mwanamume…nilishindwa tu kuwawinda na kuwaua, lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia silaha yoyote kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua…

“Ndani mwangu nilijisemea kamwe sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote anayekuja kwangu nammaliza. Kwa namna walivyoniambukiza lazima niwaambukize’.

"Sijui nimewaambukiza wanaume wangapi, lakini ni maelfu,” alisema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria hivi karibuni.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

 

ISOMe na hII

UWOYA AVURUMISHA TIMBWILI KUBWA KWENYE NYUMBA YA MUME WA MTU.

 

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top