Na Waandishi Wetu
MGOMBEA wa nafasi ya urais kwenye Klabu ya Simba, Michael Wambura, ameonyesha kuwa yeye ni kiboko yao baada ya kukata tena rufaa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wambura aliwasilisha rufaa yake kwenye Kamati ya Rufaa ya TFF, jana, akipiga kitendo cha kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa madai kuwa alipiga kampeni kabla ya muda wake.
Wambura ambaye anapambana kwa karibu na mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Evans Aveva, alitangazwa kuondolewa kwenye kinyang’anyiro, juzi, zikiwa ni siku chache tangu arudishwe na Kamati ya Rufaa ya shirikisho hilo baada ya awali kuondolewa kwa kudaiwa kuwa siyo mwanachama halisi wa klabu hiyo.
Hata hivyo, baada ya kurejeshwa, kamati hiyo ya uchaguzi ilisema kuwa imemuondoka Wambura kuwania nafasi hiyo kutokana na kupiga kampeni kabla ya muda halisi.
Akizungumza na Championi Jumatano mmoja wa watu wa karibu na Wambura alisema kuwa mgombea huyo alipeleka rufaa yake TFF, jana mchana.
“Wambura amekata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya TFF kupinga kuondolewa tena na Kamati ya Uchaguzi ya Simba, anaamini kuwa lazima haki yake ipatikane,” alisema mtu huyo wa karibu zaidi ya Wambura.
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini aliliambia gazeti hili kuwa Wambura amepeleka rufaa hiyo na kuna tetesi itasikilizwa Alhamisi jioni.
“Ngoja tuone, lakini ni kweli kuwa kuna rufaa ya Wambura imeshafika TFF na kuna uwezekano keshokutwa (kesho) tukakaa kuijadili,” alisema.
HABARI ZAIDI JUU YA SAKATA HILI BONYEZA HAPA
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment