Akiongea na paparazi jana Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani humo.
Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na kukimbilia nyumbani kwao.
"Nimemkuta yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi” alisema mama wa mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.
Paparazi ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment