Saturday, June 7, 2014

Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini ghafla.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .

Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’

Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC kilishinda uchaguzi huo.

Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa ajira.

Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.


Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top