Wednesday, June 18, 2014

Rage: Chonde Chone Malinzi Uache uchaguzi pale pale.


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.

Na Waandishi Wetu
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, amemuomba Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, kutengua maamuzi ya kusitisha tarehe ya uchaguzi wa timu hiyo na kuuacha ufanyike siku iliyopangwa tangu awali.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Kauli hiyo ya Rage inakuja siku chache tangu Malinzi kuzuia uchaguzi wa timu hiyo huku akiitaka Kamati ya Utendaji ya Simba kuteua kamati yao ya maadili, itakayopitia rufaa za wagombea na wanachama zilizowekwa.

Maamuzi hayo ya Malinzi, pia yaligomewa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya mwenyekiti wake, Dk Damas Ndumbaro ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
Akizungumza na Championi Jumatano, Rage alisema tayari ameiandikia barua TFF akiomba kuacha uchaguzi wa timu hiyo ufanyike Juni 29 kama ilivyopangwa, kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Masaki jijini Dar es Salaam.

“Kwanza kabisa ninaomba kukanusha taarifa zilizozagaa kuwa, nimevunja kamati ya uchaguzi, siyo kweli, kamati nimeichagua mwenyewe, haitawezekana kuivunja, badala yake itaendelea kubaki kama ilivyokuwa mwanzo hadi mchakato wa uchaguzi utakapomalizika.
“Pia ifahamike kuwa kamati ya maadili haipo na sijaiunda Simba, hiyo ni baada ya kuwepo TFF, nikiamini kuwa uchaguzi na mengine ya kamati za maadili zitafanyika chini ya TFF kwa mujibu wa kanuni zake zilizopo,” alisema Rage.
“Mimi sijamlazimisha Malinzi kuacha uchaguzi kama ilivyopangwa, mimi nimeandika barua ya kumuomba atuachie tarehe tuliyoipanga ya uchaguzi ibaki kama ilivyopangwa ili kuleta amani na ushirikiano katika kipindi hiki ambacho Simba inahitaji kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao na sisi hatupo madarakani,” aliongeza Rage aliye bungeni huko Dodoma.
 Katika uchaguzi huo, kamati ya uchaguzi wa Simba imemuondoa tena kwa mara ya pili Michael Wambura aliyekuwa akiwania urais kutokana na kukiuka kanuni za uchaguzi, baada ya kupiga kampeni kabla ya muda wake.



Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top