Meneja wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Rashid Mauji 'Father Mauji' pamoja na shabiki wa Jahazi wakizindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama.
Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Chozi la Mama uliobeba jina la albamu iliyozinduliwa usiku huu Dar Live.
Mashabiki wa Jahazi wakifuatilia uzinduzi huo muda huu.
Khadija Yusuf akitoa burudani ndani ya Dar Live wakati wa uzinduzi wa Chozi la Mama.
MC wa leo katika uzinduzi wa albamu mpya ya Jahazi, Aisha Abushily 'Mama wa madikodiko' (kushoto) akiwa katika pozi na Leila Salim 'Aunt Liloo' wote kutoka Mombasa, Kenya.
Wadau wa Jahazi, Injinia Arnold Gabone (kushoto) na mwenzake wakiwa katika pozi wakati wa uzinduzi wa Chozi la Mama.

Burudani zikiwa zimepamba moto Dar Live.
Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake Mzee Yusuf 'Mfalme' imezindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama yenye jumla ya nyimbo sita usiku huu ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakheem jijini Dar. Albamu hiyo ni ya 10 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment