Wednesday, June 18, 2014

Majibu ya Ridhiwani Kikwete kuhusu NEC na umiliki wa vituo vya mafuta.

Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na hujawahi kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu ambayo umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana mali hizi na hizi’

‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’

Ridhiwani Kikwete‘Kuna kipindi unaweza ukashangaa Mwandishi wa habari anachukua kalamu anaandika maneno mpaka unashangaa kayatolea wapi? sitaki kuamini kwamba Mwandishi unaweza kuandika kwamba Ridhiwani kapata UNEC kwa sababu ya baba yake, ungechukua muda ukamsoma Ridhiwani vizuri ukauliza watu waliokaa na Ridhiwani, uliza huyu ameshawahi kuwa kiongozi??’

‘Wako watu ambao kwa kuwa wamemjua Ridhiwani baada ya Jakaya Kikwete kuingia Ikulu basi nao wanaanzia hapohapo Ikulu lakini hawajui Ridhiwani kabla ya baba yake hajawa Ikulu alikua anaishije, mimi nimekua naishi maisha ya kawaida nimekaa boarding school nimesoma Mkwawa baba yangu akiwa Waziri, nilikua na uwezo wa kwenda kusoma Ulaya lakini nimesoma chuo kikuu Dar es salaam pale japo nilikua na uwezo wa kwenda popote pale ninapotaka ila ni kwa sababu tu mzee wangu alitaka kuona naishi kama watu wengine’ Msikilize hapa chini:

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top