Saturday, June 14, 2014

Majibu ya Monalisa kwa waliodai anachukua ‘pole asizostahili’ kufuatia kifo cha George Tyson

Monalisa akiwa na binti aliyezaa na George Tyson, Sonia 

Muigizaji wa filamu nchini Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ambaye pia aliwahi kuwa mke wa marehemu George Tyson aliyefariki dunia kwa ajali ya gari wiki kadhaa zilizopita, amefunguka kupitia Instagram kuelezea kusikitishwa kwake na ‘majungu’ ya watu kuwa hakustahili kupewa pole kufuatia msiba huo.
Monalisa ameandika:
Let me clear the air.ni hivi,pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George ktk maisha yetu,kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwengine..bt kwa macho ya kiMungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala.anayesema mke wa tyson alijifungia ndani mm nikawa nachukua pole zisizo zangu,dah!kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio mmoja.na wote walijifungia ndani,kwanini?ni wakristo na wanaijua dini.waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi,ni kwann?jiulize kabla ya kuropoka halafu ww ni mwanamke kuna siku yatakukuta.nilienda kutimiza wajibu wangu kama mke,ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana,nimekaa msibani naambiwa nachukuwa pole za bure.wacha nikukumbushe maandiko…Alichokiunganisha Mungu?….;kilichofungwa duniani?…..;nikupende,nikutunze hadi kifo?….. sasa kifo kimetutenganisha.siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani?pamoja na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu esp.miaka 5 ya mwisho wa uhai wake.acheni nimlilie he was my best friend 1998-2014.nimeshare nae kitanda 2000-2006.nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu?ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu..na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini,mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe,na akifa?and for ur info..msianze anajifanya mke ss hv ili apewe mali..Sonia ni mali kubwa sana alioniachia am so happy.waaache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie.mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki?niacheni nimlilie,waacheni fans wangu walie na mm.


Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

George Tyson anatarajiwa kuzikwa Jumamosi ya June 15 kwao Kisumu Kenya.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top