Saturday, June 14, 2014

KITU KIDHANIWACHO KUWA NI BOMU KIMELIPUKA HUKO ZANZIBAR USIKU HUU NA KUUA MMOJA


Mtu 1 amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu, kurushwa karibu na msikiti, darajani Zanzibar.

Kuna taarifa ya kutokea mlipuko na mlio mkubwa mithili ya bomu umetokea maeneo ya Darajani karibu na msikiti na kujeruhi Wahadhiri waliokuwepo katika msikiti wa Darajani mara baada ya kumalizika Sala ya Isha.

Mlipuko huo unasemekana umetokea baada gari ambalo lililopita mbio na kurusha kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kwenye gari ambalo wangelitumia wahadhiri waliokuwa katika Muhaadhara ndani ya Msikiti

Kuna taarifa kwamba mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top