Friday, June 20, 2014

Alichokifanya Luis Suarez kwa England sijui kama ataendelea kucheza liver. Full Time England 1-2 Uruguay.

Mbio za kuwania ubingwa wa dunia zinazidi kushika, na hivi punde umemalizika mchezo kabambe uliowakutanisha Uruguay dhidi ya England. Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 2-1 wa Uruguay.
Luis Suarez akitoka kwenye majeruhi ya goti ameiwezesha timu kupata ushindi muhimu mbele ya England.
Suarez alianza kuifungua Uruguay kabla ya Rooney hajasawazisha, likiwa ndio goli lake la kwanza katika fainali 3 za kombe la dunia.
England wakiwa na kasi ya kutafuta goli la ushindi, Suarez tena akawashangaza kwa kufunga goli la pili kwa mkwaju mkali na mpaka refa anamaliza mpira Uruguay walikuwa kifua mbele.
Matokeo hayo yanamaanisha England wameondolewa kwenye mashindano haya, baada ya kufungwa mechi ya pili., wakipoteza mechi yao kwanza dhidi ya Italy.


Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Mpaka sasa timu kubwa za England, Spain, Australia na Cameroon zimeshaaga mashindano hayo.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top