Kufuatia ushindi huu wa mabao 2-0 mikononi mwa Chile
mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania sasa wamehakiki tikiti za
ndege kurejea nyumbani pamoja na Australia .
Hii ni baada ya Uholanzi kushinda mechi yake ya pili na kuongoza kundi B ikiwa na alama 6 sawa na Chile.Chile na Uholanzi hata hivyo zitakutana katika mechi ya kuamua yupi kati yao ataongoza kundi hilo.
Mshindi wa pili katika kundi B atachuana na bingwa katika kundi A inayojumuisha wenyeji Brazil na washindi wa pili katika kundi hilo Mexico.
Kwa upande wao Uhispania ambao sasa wamefungwa jumla ya mabao 7 watachuana na Australia katika mechi ambayo haitakuwa na umuhimu wowote .
Magoli ya Chile yamefungwa na E. Vargas 20', C. Aránguiz 43'
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment