Sunday, April 6, 2014

Jussa amjibu Kinana kuhusu Katiba ya Zanzibar.

kizungumza na gazeti hili bungeni mjini Dodoma jana, Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, alisema licha ya Watanzania kuahidiwa kutatuliwa kwa kero, katika vipindi mbalimbali vya urais, kero za Muungano zimeendelea kuwepo.\Dodoma. Siku chache baada ya Katibu Mkuu wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana kutaka watu wajilaumu kwa Katiba ya Zanzibar, Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ismail Jussa, amefananisha kauli hiyo na kuzika kichwa mchangani wakati mw

Akizungumza na gazeti hili bungeni mjini Dodoma jana, Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, alisema licha ya Watanzania kuahidiwa kutatuliwa kwa kero, katika vipindi mbalimbali vya urais, kero za Muungano zimeendelea kuwepo.

“Ahadi za kushughulikia kero za Muungano zimekuwa ni hewa na haziwezi kushughulikiwa kwa sababu Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Muungano,” alisema.

Jussa alisema msingi mkuu wa sheria katika Jamhuri ya Muungano ni hati ya makubaliano ya Muungano.

“Kwa hivyo, katiba zote mbili zinapata uhalali wake kutokana na hati ya makubaliano wa muungano. Anaposema Kinana kuwa Katiba ya Zanzibar inapaswa kuwa Sheria ya Muungano siyo sahihi,” alisema.

Alisema hakuna Katiba iliyowahi kutamka kuwa Tanzania ni nchi moja, isipokuwa ya mwaka 1977.

“Dhana ya Tanzania ni nchi moja ni ya muda mfupi, haitafsiri makubaliano ya Muungano kwa sababu hapana mahali popote katika hati ya makubaliano ambayo imetamkwa kuwa Zanzibar na Tanganyika zimeacha kuwa nchi ama zimefutwa,” alisema.

Jussa alisema hata kabla ya kupitishwa kwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, Katiba ya mwaka 1979 ambayo ni katiba ya mwanzo baada ya mapinduzi, inamtaja Rais wa Zanzibar kama mkuu wa nchi.

“Sasa cha ajabu nini hapo? Ibara ya kwanza ndiyo ilirekebishwa na kuwa Zanzibar ni nchi, lakini kabla ya hapo vifungu vingi vilikuwa vikisema Zanzibar ni nchi,” alisema na kuongeza.

“Ibara ya tisa ya Katiba ilikuwa ikisema Zanzibar itakuwa ni nchi ya kidemokrasia inayofuata misingi ya kijamii.”

Alisema suala la kudai serikali tatu halikuanza leo bali tangu mwaka 1964 palipotokea tatizo la ushirikiano kati Tanzania, Zanzibar na Ujerumani. Pia mwaka 1965, kulitokea sarafu na kwamba kadhia kubwa ilitokea 1971, ambapo hayati Sheikh Abeid Karume alionyesha kutoridhika na uendeshaji wa mambo ya muungano.'

ili uko nje.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top