Tuesday, March 25, 2014

Prof. Lipumba asusia uteuzi wa Samuel Sitta, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi!


Prof. Lipumba ameusiasia uteuzi huo baada ya kujikuta wenyeviti wa karibu kamati zote na bunge hilo maalum ni kutoka Chama cha Mapinduzi isipokuwa Hamad Rashid wa CUF, na kamati hiyo ya uongozi ndiyo inayoanga ajenda, kitendo cha Lipumba kuongoza kamati hiyo, ni kumtumia yeye kama boya la kuhalalisha jinsi CCM ilivyoliteka na kulihodhi Bunge hilo Maalum, hivyo hana imani na kamati hiyo ya uongozi, hivyo ameonenea bora abaki back bencher wapambane kwa hoja!.

Mwenyekiti Sitta amekubali Prof. Lipumba, kukataa uteuzi kwa sababu ni haki yake na hiyari yake kukubali au kukataa!, akajitetea, aliyewachagua hao wenyeviti sio yeye, na suala la uingi wa CCM, hauepukiki, na akatangaza hata kura zikipigwa, CCM ndio watashinda, ndio wengi, wengi wape!.
Mapalala akalalamikia, wana CCM kuhodhi karibu kamati zote!.

Lukuvi akasimama na kudai ni wapinzania wenyewe ndio hawakujitokeza kugombea!, mbona Hamad Rashid kajitokeza na kachaguliwa kwa kura nyingi!.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top