Thursday, March 27, 2014

Jini Kabula atakiwa akafanye biashara ya kujiuza ‘ukahaba’ nchini China.

STAA wa Bongo Movies, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa amekuwa akipigiwa simu na mtu asiyemfahamu na kumtaka akafanye biashara ya kujiuza ‘ukahaba’ nchini China.

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

Akizungumza na paparazi wetu, Jini Kabula alisema katika maisha yake anaamini maisha mazuri hata Bongo yanapatikana hivyo licha ya kutangaziwa dau la maana lakini amekataa.

“Nimekuwa nikipigiwa simu mara kwa mara na mwanamke mmoja ili niende nchini China kujiuza lakini nimekuwa nikimkatalia, najitambua mimi sikubali,” alisema Jini Kabula.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top