Thursday, March 27, 2014

Huu ndio uchafu wanaofanya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel.

Uchafu! Picha za madiva wakubwa wa filamu Tanzania, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson zimebambwa na gazeti hili hivi karibuni wakiwa katika hali ya kimalavidavi licha ya kwamba, mmoja ni mke wa mtu, mwingine mchumba.

Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako Wema na Aunt wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao mpya ya Familia.

Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa sasa wapo ‘klozdi’ kiasi cha watu kuwa na maswali vipi kuhusu Kajala Masanja, walipiga picha hizo wakidhamiria kuzifuta baada ya kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha hizo zikanaswa na paparazi wetu.

Staa wa filamu

Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya simu wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu hadi kupiga picha hizo ambapo Wema anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la Aunt huku naye akiwa amelegeza macho kusikilizia.

Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza kufanya kazi, tunaanza utani. Halafu kwetu mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”

Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya mume wake licha ya kutotoa tamko lolote.
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na kufikiri upya kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema. Wengi wanaamini si sahihi kwake kwa vile haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote ‘hawajatulia.
Tanzania, Wema Isaac Sepetu
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top