MABOMU ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela,
Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa -
Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende
kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.
Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji
wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali
sehemu za siri na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo
wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa
wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao
walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,
Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao
ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi
kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.
Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment