Baadhi ya wananchi waliozungumza nana mwandishi wetu walisema wanatamani kujiunga.
“Mimi nataka kujiunga na kanisa hilo kwa sababu tunataka wokovu,” alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Amos.
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Mandade alisema ana hamu ya kujiunga na kanisa hilo kwa sababu zake binafsi.
Kanisa la Rabboni Centre Ministries lina makao yake makuu Pretoria nchini Afrika Kusini na linaongozwa na mtu anayejiita Mchungaji na Nabii Daniel Lesego ambaye alilianzisha mwaka 2002.
Wakati wa mfungo waumini wa kanisa hilo wametajwa kuwa huwa wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo kwa imani kuwa Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.



0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment