Tuesday, January 21, 2014

Kumbe Rose Ndauka alikuwa anatoka na Tunda Man kabla Hajapata bwana wa sasa.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose Ndauka,ambaye waliachana tangu 2006.


Akizungumza na XXL ya Clouds Fm leo Tunda amesema walikuwa wakikutana na mwanadada huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea kuanza mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh kila kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana kabla, hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja anafanya issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi nikikutana nae, nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye kwasababu na yeye sasa hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie zangu kama vipi namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top