Friday, December 12, 2014

Pale ambapo operator anajikuta akiweka picha za utupu katika bango uwanjani.

Ajali popote, huyu jamaa amepata ajali kazini tena huenda katika mazingira ambayo hakuwahi kutarajia.

Kutokana na sheria kali za China, hii haikuwa makusudi lakini kwa sababu tayari kashafanya kosa anastahili hukumu.

Tumezoea kuona mabango ya kisasa katikati ya Miji kama Dar ambayo yanakuwa yanaonyesha picha kama Tv ambapo picha zinazoonekana kuwa zinabadilika badilika.

Nje ya Uwanja wa Maryland, Langzhou China jamaa anayehusika kuoperate bango moja amejikuta akiwa na hatia ya kukaa jela kwa siku 15 pamoja na na kulipa faini ya kiasi cha Yuan 3000 za China zaidi ya Dola 484 kwa kosa la kuweka picha za wasichana wakiwa tupu kwenye bango lililopo nje ya uwanja huo.

Japo walinzi waliwahi kuchomoa waya wa umeme kulizima bango hilo haikusaidia, watu walioshuhudia picha hizo zikionekana kwa  sekunde 12 walirekodi video na picha ambazo walianza kushare kupitia mitandao ya kijamii.

Mhandisi wa Kampuni inayohusika na kuweka mabango hayo naye pia amekamatwa japo hukumu yake bado haijafahamika.

LULU AMUWAHI IDRIS; ASEMA ANA URAFIKI NAE.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online