Saturday, November 15, 2014

UNYAMA!! MWANAMKE MGONJWA ABAKWA NA WAFANYA KAZI WA HOSPITALI NDANI YA HOSPITALI YA SERIKALI.

Mwanamke nchini Pakistan Polisi nchini Pakistan wanawashikilia wanaume watatu kwa kosa la utumizi dawa za kulevya na ubakaji kwa mgonjwa aliyefuata matibabu katika hospitali ya serikali. Mwanamke huyo, ambaye alijifungua hivi karibuni,alikwenda katika eneo la Burewala Mashariki ya jimbo la Punjab,iliko hospitali hiyo na alikwenda hapo akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao mchanga kwa uchunguzi wa kitabibu.

Mume wa mwanamke huyo alimwacha mkewe kitambo kifupi tu na aliporejea eneo alipokuwa ,hakumkuta ila mtoto na begi la mwanamke huyo vimetelekezwa. Saa kadhaa baadaye,alimpata mkewe akiwa amelala katika chumba chenye kiza ,kilichomo katika hospitali hiyo na kuthibitika kuwa amebakwa .

 Baada ya fahamu kumrejea mwanamke huyo alisema kwanza alichomwa sindano na wanaume hao watatu kisha wakaanza kumbaka kwa zamu. Wanaume wote hao ni wanafanya hospitalini hapo.

Wema Sepetu Releases Picha kali sana Baada ya kuzinguana na Jamaa, Zicheki Hapa kweli Kaumbika



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top