Sunday, October 19, 2014

Yanga 0-0 Simba, watani wa jadi washindwa kufungana.

MPAMBANO wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga umemalizika katika uwanja wa taifa Dar es Salaam kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0 mchezo huo ukivunja rekodi kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi zaidi tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu.

Sare hiyo imeifanya Yanga kushindwa kuvunja uteja na kulipa kisasi cha kufungwa idadi kubwa ya mabao kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Simba ambao walikuwa hawapewi nafasi ya kupata angalaui pointi moja katika mchezo huo kulingana na ukali wa kikosi cha Yanga.

Sare hiyo imekuwa ni ya nne mfululizo kwa Simba inayofundishwa na kocha Mzambia Patrick Phiri na haijawahi kupata ushindi tangu kuanza kwa msimu huu lakini matokeo hayo yameifanya Yanga kushuka hadi nafasi ya nne baada kwa kufikisha pointi saba nyuma ya Azam na Mtibwa Sugar zenye pointi 10.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Yanga lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia vizuri nafasi hiyo ambayo ingeweza kuwapatia bao la mapema.

Katika dakika ya sita mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi alifanikiwa kuwalamba chenga mabeki wa Yanga lakini akatoa pasi ya ovyo kwa mshambuliaji Elias Maguli na mpira kudakwa na kipa wa Yanga Deogratius Munishi.

Yanga ambayo ilianza taratibu mchezo huo ilionekana kuzinduka katika dakika ya saba ambapo mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’aliunganisha kwa kichwa krosi ya Mrisho Ngasa lakini mpira ukatoka nje sentimeta chache kwenye lango la Simba.

Jaja ambaye katika mchezo huo alikuwa akikabwa vilivyo na mabeki wa Simba Joseph Owino na Hassani Ishaka katika dakika ya 13,alikaribia kuifungia timu yake bao kufuatia shuti kali alilopiga baada ya kurushiwa mpira na Oscar Joshua lakini kipa Manyika Peter akaliona na kulidaka.

Mchezo huo uliendelea kuwa wavuta nikuvute kwa timu zote mbili kutengeneza nafasi kadhaa za magoli na kushindwa kuzitumia katika dakika ya 16 Emmanuel Okwi,alijaribu kupiga shuti kali kwenye lango la Yanga akiwa nje ya 18 lakini halikuweza kulenga lango.

Katika dakika ya 30 Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Said Ndemla na nafasi yake kuchukuliwa na Shabani Kisiga,mabadiliko hayo hayakuweza kuubadili mchezo kama vile ambavyo ilitarajiwa kwa sababu hakuweza kuisaidia sana timu hiyo kama ilivyo kwa kiungo Mkude,ambaye alitolewa kupindi cha pili baada ya kuumia bega.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza mwamuzi Israel Nkongo,aliwaonyesha kadi ya njano wachezaji Ishaka wa Simba na Ngasa wa Yanga baada ya kutaka kupigana uwajani wakati pambano likiendelea.

Kipindi cha pili Simba ilikianza kwa kasi tena na kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Yanga lakini haikuweza kupata bao licha ya Maguli kupata nafasi ya wazi dakika ya 46 lakini kichwa chake kilikwenda nje.

Mshambuliaji wa Yanga Andrey Coutinho naye aliikosesha ushindi timu yake kufuatia kupata nafasi tatu za wazi akiwa na kipa lakini mashuti yake hayakuweza kulenga goli na mengine yaliokolewa na kipa Manyika wa Simba.

Mchezo huo uliendelea kuwa na ushindani mkali Yanga ilionekana kubadilika na kukitawala kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 71 Okwi alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Simon Msuva.

Katika dakika za mwishoni mwa ipindi cha pili Yanga ilionekana kupania kuondoka na pointi zote tatu baada ya kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Simba lakini hawakuweza kupata bao

Kuona hivyo Yanga ilimtoa Jaja dakika ya 82 na kumuingiza Hamisi Kiiza na Simon Msuva aliyechukua nafasi ya Haruna Niyonzima lakini hadi dakika 90 zinakamilika wachezaji hao hawakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo.
CHANZO: GOAL.COM

PICHA MBALI MBALI ZA DAVIDO AKAMUA SERENGETI FIESTA DAR.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top