Tuesday, October 21, 2014

WANAWAKE WA 4 KUFIKISHWA KIZIMBANI KWA KUCHEZA NGOMA ZA KIGODORO WAKIWA WATUP.


WAKAZI wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara wamefikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani kujibu shitaka linalowakabili la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya vigodoro kwenye sherehe ya ndoa.
Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (Jina linahifadhiwa) walifikishwa mahakamani hapo juzi mbele ya Hakimu Halfani Ulaya na kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Iddi Athumani.

Athumani alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika eneo la Masasi Mbovu huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa linalokwenda kinyume na maadili ya kitanzania.

Alidai kwa kuwa shauri hilo linamshirikisha mtoto aliye chini ya miaka 18, ni vyema Mahakama ikaahirisha kesi hiyo ili kupisha upelelezi wa kina kuhusu shitaka hilo linalowakabili washtakiwa hao.

Hakimu Ulaya alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka na aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 30 mwaka huu itakapotajwa tena. Watuhumiwa hao walio nje kwa dhamana hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo.
CREDIT: BOSS NGASA.

BI HARUSI ATOROSHWA, MAMA MZAZI AHAHA!



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top