Saturday, October 25, 2014

ROSE MUHANDO MGONJWA ANAHITAJU MAOMBEZI YAKO.

UMUOMBEE! Hali ya kiafya ya staa mkubwa wa Injili Bongo, Rose Muhando siyo nzuri na amewaomba Watanzania wamuombee kwani ni mgonjwa.

Staa mkubwa wa Injili Bongo, Rose Muhando.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum katikati ya wiki hii, Rose ambaye ameripotiwa kwa misala tofauti ya kuchikichia fedha za shoo hivi karibuni, amefunguka kuwa afya yake si nzuri kwani anasumbuliwa na mshipa kwenye mguu, akafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma.

“Siko vizuri kiafya nimefanyiwa upasuaji mguuni, nimeshonywa nyuzi nne lakini bado hali yangu si nzuri kiafya, nawaomba Watanzania waniombee,” alisema Rose kwa tabu na kuongeza:

“Hata ukiniona utanihurumia kwani mbali na upasuaji kwenye kidole gumba pia nimevimba sana uso.
“Kwa sasa nipo kitandani nyumbani kwangu najiuguza. Nitarudi tena hospitalini Jumanne ijayo.”
Akizidi kumwaga maneno kwa kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Rose alimshukuru mwandishi wa Barua Nzito iliyochapishwa katika gazeti tumbo moja na hili la Risasi Mchanganyiko (toleo lililopita) kwa kumuonya juu ya suala la kudaiwa kuingia mitini na fedha tofauti za shoo na kuomba radhi kwa Watanzania.

“Nawaomba sana radhi wote niliowakosea, niwaombe waniombee nipone na nitarejesha fedha zao,” alisema Rose.

Tunamuombea Rose kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema ili aendelee na huduma ya kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo za Injili-Mhariri.

WEMA ANAPONDA RAHA NCHINI CHINA MCHEKI HAPA.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top