Sunday, October 12, 2014

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu na kumwambia aache kumfuatafuata.

Jacqueline Massawe Wolper.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkongo huyo ambaye anajitapa kuwa ameshatembea na baadhi ya mastaa Bongo akiwemo Wolper, alikaririwa katika gazeti hilihili akidai ametembea na Wolper kisha kumwaga na sasa anammendea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema anamshangaa mwanaume huyo amekuwa akimfuatafuata na kumzungumzia katika vyombo vya habari wakati hana hadhi ya kuwa na mtu kama yeye.

“Kwangu mimi huyo mwanaume siyo hadhi yangu, ni mshamba, limbukeni asiyeweza kuniweka mjini…kifupi nimwambie akome kunizungumzia mimi siyo taipu yake, atafute wa saizi yake,” alisema Wolper na kuongeza:

“Nilikutana naye Nairobi aliposema ana shida ya kikazi ndiyo akaanza kuleta mambo ya kunitongoza, nilipomfuatilia nikaona si mtu mzuri, hazimo kidogo. Huwezi kuwa mwanaume ambaye unaropokaropoka hovyo, mimi nina mtu wangu namuheshimu, akome kunizungumzia.”

Huyu ndio mtoto ambae Polisi wa Kenya wamemuokoa akija kuuzwa Tanzania. (picha na maelezo).



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top