Thursday, October 16, 2014

HIZO NDIZI HALI ZA MAJERUHI WA MOTO WA PETROLI MBAGALA WALIOLAZWA MUHIMBILI.





Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa  wodini.

MAJERUHI 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.

Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.

Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni  Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).

Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.

UZINDUZI MAALUM WA NGUO ZA T.I WATANGAZWA DAR.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top