Tuesday, October 21, 2014

BI HARUSI ATOROSHWA, MAMA MZAZI AHAHA!


KAZI sana! Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.
Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.

Bi harusi mtarajiwa, Saida Said (18) aliyetoroshwa siku chache kabla ya ndoa.

Akizungumza na Uwazi juzi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake lichapishwe gazetini alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila akimpigia simu hapatikana hewani.

Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.

Muonekano wa karibu zaidi wa binti Saida Said.

“Mpaka sasa mama wa bi harusi hajatoa taarifa kwa bwana harusi wala ndugu zake, amekuwa akimtafuta kimyakimya huku akimuomba Mungu binti yake apatikane kwa vile mahari  alishalipwa, sasa anaogopa ikifika siku ya ndoa itakuwa aibu kubwa,” alisema ndugu huyo.

Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu;  BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.

Galatasaray have been fined €50,000 by Uefa following the crowd disturbances during their Champions League defeat to Arsenal.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top