Friday, September 12, 2014

WEMA, DIAMOND, AUNT WANATAJWA KWENYE MICHEPUKO HATARI SANA!

 Ni tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.

Mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.

KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.

AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.

Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.

AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.

Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.

‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.

WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.

KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.

'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.

STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.

I Have SE-X at least three to five times a week, I think it is okay – Actress Jennifer Oguzie.

“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.


'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.

NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.

“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao  wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.

Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.

AUNT AWA MBOGO
Baada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.

PICHA ZA AIBU KABISA ZA MAVAZI YA AKINA DADA WAKIWA DISCO YAANI KILA KITU NJE JIONEE MWENYEWE.

KUTOKA IJUMAA
Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top