Friday, September 5, 2014

UMEIPATA HII YA OKWI KUWA TAYARI KUCHEZA SIMBA HATA BURE??.

Mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi.

BAADA ya kufanikiwa kutua Simba, kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi hicho, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo bure.

Okwi amesema maneno hayo akimaanisha kuwa yupo tayari kucheza bila hata kulipwa mshahara kwa kudai kuwa hilo suala la fedha siyo tatizo kwake.

Akizungumza na Championi Ijumaa, jana, Okwi ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga na kusaini kuichezea klabu hiyo kwa miezi sita, amesisitiza kuwa anaipenda Simba na atafanya hivyo pia itakapobidi ili kulinda kiwango chake.

“Unajua sasa hivi nimebadilika na siyo Okwi yule waliyekuwa wakimjua, sitakuwa mtukutu kama ambavyo walikuwa wakinisema mwanzoni,” alisema Okwi.

Mganda huyo ameongeza kuwa anaamini yuko mahali sahihi, hivyo atahakikisha anapambana kuweka kiwango chake kuwa bora. “Nimefurahi kurejea Simba na kuitumikia timu hii, mshahara siyo tatizo,” alisema Okwi.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA


PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU 

 

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top