Mjane Stell Barlow wakati wa mazishi ya aliyekuwa mume wake, Kamanda Liberatus Barlow.
Sakata la madai kuwa mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Stella Barlow (pichani)alitimuliwa ukweni kwa mapanga limechukua sura mpya baada ya ndugu wa mumewe kuibuka na kutoa ufafanuzi.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, ndugu wa marehemu Kamanda Barlow, aliyejitambulisha kwa jina moja la Lyimo alisema si kweli hata kidogo kuwa walimkimbiza kwa mapanga shemeji yao huyo.

Kamanda Barlow enzi za uhai wake.
Alifafanua kuwa wamewahi kufanya misa ya kumuombea marehemu Barlow na ndugu wengine na mama huyo aliarifiwa lakini hakuja. “Ujumbe wetu ni kwamba muambieni huyo mama kuwa siyo vizuri kuchafua ukoo kwa sababu hatuna ugomvi naye na hakika kama ni wa kulaumiwa ni yeye siyo sisi wana ukoo,” alisema Lyimo.
Wakati huo huo, kwenye Gazeti la Uwazi la Agosti 27 mwaka huu tuliweka kimakosa picha ya mke wa marehemu Kamanda James Kombe badala ya mke wa kamanda marehemu Liberatus Barlow, Stella Barlow. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliowapata wahusika- Mhariri.

0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment