Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuwasili leo jijini katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja.
Is Agatha Atiti A Hottest TV Personality In EAST AFRICA? ……..Check Out Some Of Her Sexy Photos.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia ngoma za utamaduni baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere Leo jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya ziara ya siku moja hapa nchini.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Katikati)akipata maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na kushoto ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye amewasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku moja . ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
Ndege iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment