
Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.

Pichani juu na chini malori mengine ya mizigo yakipita karibu na eneo la tukio.

Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni.
DEREVA wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo wamejeruhiwa.
Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment