Mwanaume anayejulikana kwa jina moja la Talick, anayedai kuwa ni mtoto Khadija Kopa.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Dully ambaye amekumbana na ushawishi mkubwa kutoka kwa Talick, alisema amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka jamaa huyo akimuomba urafiki wa karibu akidai hata mama yake (Khadija Kopa) ameshamwambia.
“Dah! Dunia hii! Sijui hata alipata wapi namba yangu na kuanza kunishawishi eti tuwe marafiki kwani hata mama yake, Kopa anajua, nikashindwa kumuelewa ni urafiki gani wa mwanaume kwa mwanaume,” alisema Dully.

Malkia wa mipasho bongo Khadija Omari Kopa akiwa na Talick.
Baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kopa ili kuzungumzia namna jina lake linavyotumika ambapo alisema hamfahamu huyo mtu na aache kutumia jina lake.
“Huyo mtoto mi simfahamu, amepiga picha na mimi kama mashabiki wangu wengine lakini huwa siwafahamu wote, aache kabisa ujinga wake mimi ni mtu mwenye heshima zangu,” alisema Khadija Kopa.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment