Monday, September 15, 2014

FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA.

 Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.

Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.

Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.

Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

DIAMOND PLATINUMZ "DANCERS WANGU NDO WANAOLIPWA PESA NYINGI KULIKO WOTE AFRICA"..

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top