Saturday, September 6, 2014

DK MWAKYEMBE AAMURU MAKAMPUNI YA MABASI YALIYOSABABISHA AJALI KUFUNGIWA MARA MOJA.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe (Picha na Maktaba).

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya  J4 Express  na  Mwanza Coach yafungiwe mara moja.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu muda mfupi uliopita, Dk Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39  na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.

“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha sana. Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.

UMEIPATA HII YA Canadian Millionaire KULIPIA $80,000 ili Kumkiss Mdomoni Elizabeth Hurley. Hii HAPA

Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi. “Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

BINTI ANAYEDAI KUBAKWA NA MUME WA FLORA MBASHA AIELEZA MAHAKAMANI JINSI ALIVYOBAKWA.


PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online