Tuesday, August 12, 2014

Watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa UKAWA Wampiga na kumjeruhi Vibaya mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.


MJADALA kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya, umeingia hatua nyingine baada ya Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Thomas Mgoli, kupigwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, amewaonya wajumbe wa bunge hilo, kuacha kuhamishia mijadala baa, kwani ni hatari kwa maisha yao na kuwaomba Watanzania kuwa wavumilivu katika masuala yanayohusu Katiba.

Mjumbe huyo wa Kundi la 201 anayetoka chama cha NDC, alivamiwa na kupigwa juzi saa mbili usiku katika duka la pombe (grocery) lenye jina la Lidya, lililopo Area A, jirani na Shule ya Msingi Chamwino mjini hapa na kuumizwa kwa kiasi kikubwa upande mmoja wa jicho, ambao umevimba

JACK PATRICK AYEYUKA GEREZANI NDUGU WAHAHA, HOFU YA KUNYONGWA YATANDA.

Akizungumza huku akigugumia kwa maumivu hospitalini hapo, Mgoli alidai kuwa waliompiga anawatambua kuwa ni wafuasi wa Ukawa, huku pia wakiwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwani amekuwa akizungumza nao masuala ya kisiasa katika eneo hilo mara kwa mara wakati wakinywa pamoja.

Awatambua
“Nawafahamu kwa sura hata na itikadi zao kwa kuwa tumekuwa tukikutana eneo hilo kupata vinywaji. Licha ya kubishana nao masuala ya kisiasa, lakini pia wamekuwa wakivaa magwanda ambayo ni sare ya Chadema, hivyo naijua mielekeo yao na itikadi zao kuhusu Bunge Maalumu la Katiba, nashangaa kwa nini wamenifanyia hivi.

“Mmoja kati ya walionipiga anajiita Vampire (Nyonya Damu) na nimeshakutana naye zaidi ya mara sita, tukikaa na kunywa pamoja na kujadili changamoto ndogo ndogo sikutarajia kwamba wangefikia hatua ya kunipiga,” alisema Mgoli.

DADA YAKE DIAMOND NAE AANZA KUUZA SURA MITANDAONI MCHEKI HAPA.

Akifafanua, alisema alipofika katika eneo hilo juzi alikutana na wafuasi hao, ambao walikuwa wanne na kulikuwa na mmoja ambaye ndiye alimuona kwa mara ya kwanza siku hiyo na alijitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

U-CCM
“Nilienda pale kwa nia ya kununua vinywaji, basi kwa vile huwa nawaona kwenye ile grocery, wakaanza kunitupia maneno makali wakihoji kwa nini naunga mkono hoja za CCM (Chama Cha Mapinduzi), hali hiyo ilinishitua kidogo.

“Niliwaambia nimekuwa nikichangia hoja kwa maslahi ya Taifa na nikawaeleza kuwa ni vyema hoja za kila mmoja zikaheshimiwa hata kama zinatukwaza.

“Niliposema Katiba itapatikana tu, ghafla nikashtukia nimepigwa na kitu pembeni ya jicho, kuangalia nikaona ni jiwe na watu hao wakaanza kukimbia,” alieleza Mjumbe huyo, aliyesema anaishi maeneo hayo ambako amepanga nyumba.

Sitta
Kwa upande wake, Sitta, akizungumza na Mjumbe huyo alipoenda kumjulia hali, aliwataka Wajumbe wa Bunge Maalumu kuwa makini na maeneo wanayokaa. Pia, alionya mijadala ya ndani ya Bunge wasiipeleke mitaani kwa vile huko kuna watu wenye mitazamo ya aina tofauti.

“Nilikuwa safarini ndiyo nimefika leo, nikapata hizi taarifa, nimekuja kumuangalia Mjumbe wangu, ni tukio la kusikitisha, tunataka kujenga jamii ya aina gani?” Alihoji na kuwataka wafuasi wa Ukawa, kutambua Bunge Maalumu la Katiba lipo kisheria.

“Ni vyema wananchi wakiwemo wanachama wa Chadema na Ukawa, watambue kuwa Bunge hili lipo kisheria, inashangaza kuona kuna baadhi ya watu wanataka kulizuia Bunge Maalumu la Katiba, huku wakiwa nje ya Bunge ambalo ni la kisheria,” alisema na kuomba kuwe na uvumilivu katika mijadala.

Alisema haiwezekani watu wachache, wakapinga kitu kilichopo kwa mujibu wa sheria. Alisisitiza kuwa pamoja na matukio hayo, lakini bado Watanzania watarajie kupata Katiba nzuri.

Aliwataka wajumbe, kutotishika na matukio hayo. Sitta alisema amesikitishwa na tukio hilo la kutishia amani kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu. Alisema kuwa atahakikisha sheria inafuata mkondo wake, huku usalama ukiongezwa zaidi.

“Lakini nawaomba Wajumbe ni vyema watumie Bunge kufanya mijadala badala ya kuhamisha mijadala nje ya Bunge, kwani ni chanzo cha matatizo, ufike wakati sasa mijadala hii isitoke nje ya Bunge ikiwemo maeneo ya starehe, kwani huko inaweza kuleta madhara,’’ alisema Mwenyekiti huyo.

Polisi
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alikiri kupigwa kwa mjumbe huyo. Alisema tayari watu watatu wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu shambulio hilo, huku wengine wawili wakitafutwa.

Hata hivyo, alisema alikuwa nje ya ofisi kwa jana, hivyo asingeweza kutaja majina ya wanaoshikiliwa. Aliahidi kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa habari kuhusu tukio hilo leo.


Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA.

Lady From Kisii Infects 31 Men With HIV.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top