Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa wamewekwa katika shule . Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
JIONEE BAADHI TU YA MAMBO WAFANYIWAYO MABINTI WAENDAO COCO BEACH HAPA......
Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.
Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment