
Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani.

Watangazaji hao wakiongozwa na maofisa wa polisi kuelekea mahakamani.

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.
Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment