
Mke wa Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wafugaji la Pingos Forum, Edward Porokwa, Flora Porokwa aliyepigwa risasi.
Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo risasi hiyo alipigwa kwapani na kwenda kutokea mgongoni na kulazimika kuendesha gari umbali wa kilometa moja akiwa na risasi mwilini.
PICHA ZA KIBONDE NA GARDNER WAKIPANDISHWA KIZIMBANI JANA.
Majeruhi huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Seliani jijini hapa, alionesha ujasiri wa hali ya juu baada ya kumudu kuendesha gari hilo huku watu hao wawili waliokuwa wamepanda bodaboda wakiendelea kumfuatilia hadi alipofika nje ya nyumba yake ambapo aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa anasubiri kufunguliwa geti la kuingia ndani.BAADA YA KUTIMULIWA SIMBA LOGA AVAA JINGINE SASA AMENDEA PENZI KWA WEMA SEPETU.

Jeraha la mgongoni alilopata Flora Porokwa.
Alisema mmoja wa watu hao alimfuata na kushika kitasa cha mlango wa mbele na kujaribu kufungua lakini mlango haukufunguka. Ndipo mwanamke huyo alipoamua kushusha kioo cha mlango ili aweze kumsikiliza, lakini ghafla jambazi huyo alichomoa bastola na kumpiga risasi kwapani.
“Kwenye gari sikuwa na fedha, sijui kama walilenga kunipora au kuna tatizo lingine. Nikiwaona naweza kuwakumbuka kwa sura ila siwajui, sikuwahi kuwaona kabla,’’ alisema mwanamke huyo na kuongeza kuwa:
PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.
“Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na kifo kwani dhamira yao ilikuwa kuniua.”Majeruhi huyo ambaye hali yake bado siyo vizuri, alitoa rai kwa jeshi la polisi mkoani Arusha kuwasaka watu hao kisha kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Hadi sasa tukio hilo halijafahamika undani wake kama watu hao walilenga kupora fedha au ni kisasi, kwani kabla ya tukio hilo kuna taarifa kwamba hata mumewe, Porokwa aliwahi kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Jirani mmoja wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema wamesikitishwa mno na tukio la mwenzao kupigwa risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment