Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya lori baada ya kugongana uso kwa uso.
Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya lori la mafuta.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo.

AJALI mbaya imetokea barabara kuu ya Arusha - Moshi ikihusisha lori aina ya Scania lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Picha Mpya za Rihanna ambazo W Magazine imemtambua Rihanna kama “world’s wildest style icon”.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliiambia Globu ya Jamii kuwa ilitokea majira ya saa 7 jana katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo Chuo cha Polisi Moshi kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.
Katika ajali hiyo mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya, mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, alifariki dunia papo hapo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment