Friday, August 22, 2014

MAINDA: NIMEFANYA SANA YALE MAMBO, SASA BASI!

Staa wa filamu Bongo Ruth Suka ‘Mainda’akipozi.
STAA wa filamu Bongo aliyeamua kumpokea Yesu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kipindi cha nyuma alipotangaza kuokoka alikuwa ni kama anamtania Mungu ila sasa ameokoka kikwelikweli.

DEREVA BODABODA AMNG’ATA MWENZAKE MDOMO NA KUONDOKA NAO.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema awali alipofunguka kuwa ameokoka, hakuwa siriasi kwani alikuwa akiendeleza anasa za hapa na pale lakini sasa yeye na Yesu, Yesu na yeye.

“Mwanzo nilikuwa kama namtania Mungu, nilisema nimeokoka lakini kimyakimya nilikuwa naendeleza anasa, nimefanya sana anasa lakini sasa basi.

“Huwezi kunikuta sehemu yoyote ya starehe hata siku moja, wala kuniona nimevaa mavazi ya ajabu na hata filamu nikicheza siwezi kuonekana kama mwanzo, nachagua vipande vya kucheza ambavyo haviwezi kunivua wokovu wangu,” alisema Mainda.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

ISSUE ZA MADAWA YA KULEVYA: DIAMOND KIMENUKA MBAYA; NZOWA ASEMA AMA ZAKE AMA ZAO.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top