Akielezea tukio hilo, msichana huyo ambaye sasa amejifungua, alisema shangazi yake ambaye hana msaidizi nyumbani kwake, alimpigia simu bibi yake anayeishi naye, akimuomba yeye aende kumsaidia kufua nguo.
Alipokwenda, kwanza aliambiwa atoe mbolea katika zizi la ng’ombe lakini akiwa huko, binamu yake, ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, alimfuata na kutaka kumbaka, kabla ya kufanikiwa kukimbia.
HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU
Alisema alipomweleza shangazi yake kuhusu suala hilo, alimjibu kwa kilugha akimwambia kuwa asimwambie upuuzi, kitu ambacho kilimuuma binti huyo ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15.“Niliondoka baada ya shangazi kunijibu hivyo. Nikiwa nafua nguo, Agustin aliniita ndani, nikajua ananipa zingine ili nifue, lakini nilipoingia alinishika mkono na kunivutia chumbani kwake, akaniambia ole wangu nikipiga kelele au kumwambia mtu, atanifanyia kitu ambacho sitasahau, aliniziba mdomo, akanivua ngua na kuanza kuniingilia,” alisema binti huyo.
“Nilisikia maumivu makali sana, nikamwambia shangazi, lakini hakutaka kunisikiliza, nikamweleza pia yeye mwenyewe Agustin kuwa nimeumia sana, hakunijibu. Kesho yake aliniletea dawa nimeze, nikameza nikarudi kwa bibi yangu. Baada ya miezi 6 nikasikia tumbo linauma, nikajua nina minyoo nikamwambia shangazi akanipa dawa za minyoo, nikazimeza, hata hivyo sikuona dalili za kupona.
KATANGAZE: LIVE! MSANII WA BONGO FLEVA ANASWA AKINUNUA MACHANGU Sinza Africasana Dar.
“Nikamwambia Agustin naumwa tumbo, akaniambia nioge anipeleke hospitali, nilipima nikakutwa nina mimba ya miezi 5, alinichukua akanipeleka hospitali ya Mawezi, akaongea na daktari mmoja akampa dawa, sikujua ni za nini nilipotumia nilipatwa na kizunguzungu, kumbe zilikuwa ni za kutoa mimba, pia alinipeleka Arusha Mianzini kwenda kutoa mimba kwenye dispensari iliyoko huko, akapewa dawa anipe wakati tukiwa tumefika nyumbani.”AJALI MBAYA KABISA YA MABASI KUGONGANA USO KWA USO YAUA TAKRIBANI 16 NA KUJERUHI 75 TABORA.
Najma alipatikana na kukiri kwenda Moshi kumfuata binti huyo, lakini alipofika naye Dar, rafiki yake alipigia simu na kumtaka amdhuru binti huyo ili kupoteza ushahidi, jambo ambalo alilipinga licha ya wito wao wa mara kwa mara.Mwenyekiti wa kijiji cha Mloe, Salutary Mushi naye alisema ni kweli Agustin ana tabia ya kupenda kutoka na watoto wadogo, jambo ambalo limekuwa kero kubwa mtaani hapo kwani huyu si mtoto wa kwanza kumharibia maisha, akidai pia kuwahi kufanya hivyo kwa mtoto wa baba yake mkubwa.
Agustin mwenyewe hakupatikana licha ya kuwepo habari za kuachiwa kutoka kituo cha Polisi Moshi alikopelekwa kwa kosa hilo lililofunguliwa kwa faili namba MS/RB3336/014.


0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment