
Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza >> ‘upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao’
PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.
Mswada huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.

Sio kila mmoja anakubaliana na ndoa za jinsia moja hata katika nchi zilizoendelea ambazo Marais wake wanaunga mkono ndoa hizo
Muswada huo pia unapendekeza kupigwa mawe hadharani hadi kufa kwa mtuhumiwa anayepatikana na kosa la kuwalawiti watoto wadogo au anayefanya kitendo hicho na kumuambukiza mtoto virusi vya ukimwi ambapo tayari wabunge 78 wamekubali kuunga mkono muswada huo kuwa sheria na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa.
SEE HOW BROCK LESNAR DECIMATESS JOHN CENA TO CLAIM HE IS THE WWE WORLD HEAVYWEIGHT CHAMPIONSHIP.
Haya yanajiri wakati Bunge la kitaifa la Kenya likibuni kikundi mseto cha wabunge kuhusu maisha ya walio katika uhusiano wa jinsia moja na wameahidi kutoa mwelekeo wa jinsi ya kushughulikia jambo hilo huku muswada huu ukitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu.Katiba ya Kenya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.
Baada ya kuisoma hii stori unaweza kuacha maoni yako kwenye comments hapa chini.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment