Tuesday, August 5, 2014

KIKONGWE AISHIYE KWA KULA UDONGO APEWA MSAADA.


KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha sana, kikongwe mmoja aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu, Uwazi limemvumbua.

Athuman Ngusa Kulaba amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi.

Kikongwe huyo alikutwa na gazeti hili hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Hii ni nyumba anayoishi kikongwe huyo, Bw. Athuman Ngusa Kulaba.

Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani  zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo.
Uwazi lilishuhudia sehemu kubwa ya ukuta wa nyumba anayoishi kikongwe huyo ikiwa imemeguka kwa ajili ya kuchimbuliwa na kuliwa.

Bw. Athuman Kulaba akionesha jinsi anavyovuna udongo kutoka katika nyumba yake kuandaa 'menyu'.

Majirani walilieleza gazeti hili kwamba, nyumba anayoishi kikongwe huyo aliachiwa kuilinda na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Musada karibu miaka 20 iliyopita bila kupewa huduma nyingine zikiwemo fedha.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed Katungi akikabidhi msaada wa chakula kwa Bw. Athuman Kulaba.

Akizungumza na Uwazi kwa lugha ya Kisukuma, kikongwe huyo alikiri kuwepo kwenye nyumba hiyo kwa miaka 20. Alisema awali alikuwa akipewa pesa na tajiri yake lakini baadaye utaratibu huo ukafa hivyo kwa sababu ya kukosa pesa ya kujikumu ndiyo akaamua kula vyakula vya ajabu, ukiwemo udongo wa ukuta wa nyumba hiyo.

Dada etu Agnes Masogange azidhi kukoleza Utam Instagram kwa kaka zetu mnaokesha Kwenye Mtandao huo.

Alisema anawashukuru majirani wa eneo hilo ambao wameweza kutambua maisha magumu anayoishi na kuamua kumpeleka hospitali na kumsaidia chakula.“Kwa sasa naomba Watanzania wenzangu wanisaidie nauli ili niweze kurudi kwetu Bukene, Tabora, maisha hapa ni magumu sana,” alisema kikongwe huyo.
Kwa Watanzania watakaoguswa na maisha magumu ya mzee huyo wanaweza kumsaidia nauli kwa kutumia namba ya simu ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed Katungi 0784 295833 au 0715 295833.
Bw. Athuman Kulaba amkishukuru mwandishi kutoka Global, Bw Denis Mtima (kulia) pamoja na Menyekiti (Mohamed Katungi) kwa msaada alioupata.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

ISOME NA HII

Dillish Mathew's exposing her smooth body in a lovely bikini outfit..

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top