YAMETIMIA! Kundi lililojipatia umaarufu mkubwa la wasanii na waigizaji la Bongo Movie Unity, limeanza kumeguka baada ya Katibu wake, William Mtitu kujiuzulu nafasi hiyo, akimtuhumu kiongozi wao kuwatumia kisiasa.

Katibu wa Bongo Muvi, William Mtitu.
“Nimechoka kutumiwa kisiasa bila ridhaa yangu, kisingizio Bongo muvi, hiyo kitu hakuna kama kuna mtu au chama kinahitaji kututumia wasanii au kuitumia Bongo muvi basi unatakiwa uwazi na si kumtumia mtu mmoja kwa manufaa yake mwenyewe,” alisema Mtitu alipoulizwa kulikoni.
PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, 'Steve Nyerere'.
Inadaiwa kuwa chombo hicho, kinatumiwa na mmoja wa watu wanaotajwa kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Urais katika uchaguzi mkuu mwakani na kwamba amekuwa akitoa fedha nyingi, ambazo zinadaiwa kuishia hewani bila kueleweka zinavyotumika.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment