Sunday, August 3, 2014

Christina Shusho,Flora Mbasha,Upendo Nkone na Rose Muhando watoa burudan kwenye Shereke za Kusherekea Helikopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima.


 Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.

Flora Mbasha akiimba katika kanisa la Gwajima.

Halima Mdee akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa hilo.

Mchungaji Gwajima akicheza kwa shangwe.

Rose Mhando akicheza kwa hisia na shangwe kubwa.

Umati wa watu waliohudhuria misa hiyo wakifuatilia kwa makini.

Upendo Nkone akiimba kwa hisia kali.

Gwajima (kushoto) akicheza pamoja na Christina (Kulia).

WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta.

Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma  sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.

Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.

Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top