MWIGIZAJI wa filamu anayekuja juu nchini, Aisha Bui, amesema ili kuyashinda maisha magumu Bongo, ni lazima uwe mkakamavu, kama yeye alivyolazimika kwenda kutengeneza filamu yake mpya ya Mshale wa Kifo, katika msitu wa kutisha ili kwenda tofauti na wengine.

Mwigizaji wa filamu anayekuja juu nchini, Aisha Bui.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, najua nina deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema mwigizaji huyo.
Alisema maoni mengi ya watu yanaonyesha wanakerwa na kila filamu kuigizwa mijini tu, hivyo yeye akajitoa ili aende sambamba na mahitaji ya mashabiki wake, kwa kwenda katika misitu ya Morogoro vijijini kuifanya filamu hiyo, aliyowashirikisha pia Mzee Chilo, Salim Ahmed ‘Gabo Zagamba’ na wengineo, kazi iliyofanywa Yuneda Entertainment.
HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment