Saturday, July 5, 2014

Wanawake watatu wakamatwa kwa kusaidia kutekwa kwa wasichana wakiwadanganya kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.

Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake watatu ambao walikua wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa kundi la Boko Haram.

Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.

>Mwaandishi wa BBC Will Ross akiwa Abuja anasema inaelekea Boko Haram inajaribu kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika mapambano yao.

Mwezi uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa mhanga alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya kijeshi katika jimbo la Gombe - tukio la kwanza aina hiyo nchini Nigeria.

Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.

Wanawake pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na kuzuiliwa katika miji ya Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram wanaungwa mkono kiasi .

Jeshi la Nigeria limewakamata wanawake wafuasi wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi la Boko Haram.

Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji wa Boko Haram.

Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa Chibok katika jimbo la Borno .

Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao waachiliwe kwa kubadilishana na wasichana.Serikali imelikataa dai hilo.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top