Monday, July 14, 2014

UJERUMANI YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA DUNIA KWENYE ARDHI YA BRAZILI.


Kocha wa Ujerumani, Joachim Low akinyanyua juu Kombe la Dunia.

Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya nne nchini Brazil usiku huu.
Mario Gotze akiifungia Ujerumani bao pekee na la ushindi dhidi ya Argentina usiku huu.


Aliyekuwa mchezaji wa Barcelona, Carles Puyol (kushoto) na modo wa Brazili, Giselle baada ya kuleta Kombe la Dunia uwanjani kabla ya mechi ya fainali kati ya Argentina na Ujerumani kuanza.

Meesi na Neuer wakiwa na tuzo zao.

TIMU ya Ujerumani imetwaa Kombe la Dunia 2014 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina katika muda wa nyongeza baada ya suluhu kwenye muda wa kawaida wa dakika 90.

Bao hilo lililoipa ushindi  Ujerumani limefungwa na Mario Gotze dakika ya 113 ya mchezo na kuifanya timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia mara ya nne baada ya mwaka 1954, 1974 na 1990.

Katika michuano hiyo, kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer ametwaa tuzo ya kipa bora, Lionel Messi wa Argentina akitwaa tuzo ya mchezaji bora huku mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez akiwa ndiye mfungaji bora baada ya kutia kambani mabao sita.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top