
Mwanamke huyo baada ya kujifungua akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wanamhudumia.

Magari ya huduma yakiwa yamefika kumchukua mama na mwanawe katika duka la Primark.
Mama huyo alijifungua salama-salmin mtoto wa kike baada ya kuzidiwa uchungu akiwa kando ya barabara. Wapita njia waliokuwa wakipita mtaani majira ya saa nane alasiri walimtafutia gari la wagonjwa, wakamwekea mablanketi chini na kumzungushia mashuka mama huyo ambaye alikuwa amelala chini ili kumsitiri.
Watu wengi walifikiri kulikuwa na onyesho fulani mtaani hapo, lakini wakagundua ni mama huyo alikuwa amejifungua. Mama na mtoto walipelekwa Birmingham City Hospital kwa huduma zaidi.
CHANZO: MIRROR
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment