Mwanaume mmoja amebakwa katika barabara ya daraja lenye shughuli
nyingi mjini Newcastle baada ya kukubali kupanda lifti ya mtu asiyemjua.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 aliingia kwenye gari hilo dogo
mapema alfajiri ambapo alifanyiwa kitendo hicho cha ubakaji katika eneo
lenye nyasi nyingi karibu na daraja la Redheugh, Newcastle.
Timu ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji hivi sasa inaendesha msako wa
mtu aliyetekeleza kitendo hicho na kuwataka mashuhuda kujitokeza
hadharani.
Afisa upelelezi kutoka mji wa Newcastle, Caroline Ord, amesema hili
ni tukio baya zaidi kutendewa kwa kijana huyo ambapo sasa polisi
wanafanya kazi bega kwa bega na mtu huyo kuhakikisha wanampata
aliyetenda kosa hilo.
Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment